Watu wengi wanashindwa kujua maana halisi ya mtaji.
Wengi wanafikiri labda mtaji lazima iwe fedha, lakini kiukweli mtaji ni
zaidi ya fedha. mtaji inaweza kuwa ni vingi vingi mbali na fedha.
Mtaji ni nini?
Mtaji ni kitu chochote ambacho unaweza kutumia kuanzishia biashara
yako na kupata faida. kwa hiyo mara nyingine sio fedha inaweza kuwa ni
kitu fulani cha aina fulani, linaweza kuwa ni jambo fulani, mahusiano ,ni
watu, ni mtandao ulionao, labda ni wazo zuri sana unakuwa nalo, ama ni
jina jema katika jamii.
Kwa hiyo vyote hivi vinaweza kuwa ni mtaji wa kuanza na kudumu
ambavyo vinaweza kubadilishwa na kuwa katika form ya pesa.
Kumbe mtaji sio fedha tu.
Njia hizo ni kama ifuatavyo
1. Mtaji mbadala
Tunapozungumzia mtaji mbadala hapa tunamaanisha ni yale mambo
ambayo ingebidi utumie fedha hutatumia fedha , utatumia kwa mfano
nguvu zako mwenyewe, au jasho mwenyewe,, au maarifa fulani,au jina
mtu mwingine, au utakopa ,au kuazima , au ubunifu, ndio unakuwa tayari
umetumia mtaji mbadala. kwa mfano kipaji ulichonacho au uzoefu fulani
au uwezo binafsi uliojijengea n.k
A. Kipaji Ulichonacho:
Mfano Masanja leo hii ni maarufu sana kwa sababu ametumia kipaji
chake cha kuchekesha kuwa mjasiriamali mzuri, Hakuhitaji pesa kufanya
ujasiriamal wake.
B. Uzoefu ulionao
Hili watu hawajui kama ni mtaji mbadala utakuta wanasema '' AAah
mimi ni mwalimu tu wa chekechea'' nifanye biashara gani, akasema sina
mtaji'' nikamwambia " huna sebule? akasema 'ninayo ' nikamwambia
anzia hapo hapo, na kufikia leo hii dada Hadija ana shule 3 za
chekechea Dar es salaam
C. Maarifa uliyonayo ambayo wengine hawana
Tunaposema maarifa mbalimbali mfano leo hii watu wananilipa kwa
kusikiliza kwa sababu nina maarifa ya kutatua matatizo ya watu
waliyonayo kijasiriamali.
D. Elimu yako
Mfano una cherehani iko ndani, kwa nini usianze kushona? wamiliki
wengi wa makampuni makubwa ya ushonaji walianza hivyo hivyo
2. Kupata mtaji kwa ndugu, jamaa na marafiki
Watu wengi wanakuwa kwenye umaskini wakati wamezungukwa na
ndugu matajiri kisa wanaona aibu kuomba msaada, lakini amini usiamini
watu wengi wametajirika kupitia ndugu, jamaa na marafiki,
Mfano mtu tajiri kuliko wote barani Afrika kutoka Nigeria ndugu Dangote
yeye alivyotaka kuanza ujasiriamali aliomba msaada toka kwa mjomba
wake ambaye alimuazima kama milioni 3 hivi kwa kuwa aliona fursa
kwenye mambo ya ujenzi (cement).
Dangote akaanza kununua cement na kuuza leo hii ndugu Dangote
amekuwa bilionea ambaye amewekeza sana barani Afrika anauza
cement, unga , mchele, mafuta, sukari na saa hivi anauza mafuta kule
Africa Magharibi hata hapa Tanzania tuna kiwanda chake kule Mtwara,
Kuomba msaada sio ishara ua udhaifu bali ni ishara ya nguvu kwamba
unajiamini ndio maana unaomba msaada. kumbuka kwenye neno
UJASIRIAMALI kuna neno Jasiri pia, huwezi kuwa na mali bila kuwa
jasiri.Umezungukwa na watu waliobarikiwa usisite kuwaambia
wakusaidie ,.
3. Kujiwekea akiba
Watu wengi sana hapa kwetu Tanzania ukiwaambia weka akiba
wanakwambia mimi siwezi kuweka akiba, sina utamaduni wa kuweka
akiba,
Hivyo mi nakushauri anza leo kujifunza kuweka akiba, ni ngumu sana
kufika juu bila kuweka akiba kwa mfano kama umeajiriwa na unajua
biashara fulani inataka milioni 2 ili kuifanya na wewe mshahara wako ni
laki 4,
Kwa nini basi kila mwezi usiweke laki 1 pembeni, ndani ya miaka miwili
utakuwa na milioni 2.4 huo ni mtaji wako wewe mwenyewe.
Usisite kuanza kidogo kwa kuweka akiba polepole mpaka ufike huko
unakoenda
4. Pata Mtaji kwa njia ya kudunduliza
Hii njia ya kudunduliza ndio njia ambayo ni nyepesi kabisa ambayo watu
wengi hawaioni, ukiamua kutumia njia hii kamwe huwezi kukosa mtaji,
Hii ina maana unaanza katika hali ya chini kabisa ya kufanya kitu
chochote halafu ile faida unayoipata hauitumii bali unaiwekeza kwenye
biashara yako.
Zingatia semina niliyo kupatia anzisha biashara leo njoo inbox nikupe fursa itakayo kusaidia kuwa milionea kwa mtaji wa laki mbili Tsh:200,000.
This site was designed with Websites.co.in - Website Builder
We appreciate you contacting us. Our support will get back in touch with you soon!
Have a great day!
Please note that your query will be processed only if we find it relevant. Rest all requests will be ignored. If you need help with the website, please login to your dashboard and connect to support