IFAHAMU TEKNOLOJIA YA BLOCKCHAIN NA FAIDA ZAKE

By MZ TECHNOLOGY
Wed, 19-Oct-2022, 18:52

Blockchain ni mfumo ambao unajiendesha wenyewe kupitia internet (decentralized system) ambao unawezesha kutuma au kupokea fedha na kutunza taarifa za miamala hiyo au taarifa nyingine kama mikataba, system n.k

Decentralized system ni mfumo ambao haumilikiwi na mtu yeyote wala hauna makao makuu bali ni mfumo uliopo ulimwenguni kote na mmiliki wake ni mtu yeyote yule ambaye atautumia mfumo huo kwa mambo mbalimbali. 

Taarifa zilizopo kwenye blockchain ni taarifa endelevu ambazo ni vigumu kubadilishwa (edited) kudukuliwa (hacked), kufutwa (deleted) au kuharibiwa (destroyed) ndio maana blockchain inaitwa DISTRIBUTED LEDGER TECHNOLOGY (DLT). 

Blockchain imeundwa na blocks(boksi/tofali/faili) ambazo ndio zimehifadhi taarifa husika za watumiaji kama vile miamala iliyofanyika, muda, siku na kiasi kilichotumwa/kupokelewa na boksi hizo zimeunganishwa kwa pamoja kwa kutumia chain (mnyororo) na ndio maana mfumo huo unaitwa Blockchain. 

Taarifa hizo zilizopo kwenye hizo blocks/files zinalindwa kwa kitu kinachoitwa HASH ambayo tunaweza kusema ni kama Nywira (Password) ambapo kila block inakuwa na HASH yake na vile vile kila block inakuwa na HASH ya block iliyopita na inaitambua. Mfano tuna block A, B, C na D na zote hizo zina HASH, block B itakuwa na HASH za block A, Block C itakuwa na Hash za block B na block D itakuwa na HASH za block C hivyo basi ikitokea data za block A zimedukuliwa kila kitu cha block A kitabadilika na HASH pia itabadilika na hivyo basi block B na nyingine haziwezi kuitambua block A tena maana kila kitu kimebadilika. 

Na ili itambulikane kwa hiyo HASH hiyo mpya itabidi mdukuzi abadili taarifa zote za kila block kitu ambacho ni ngumu maana kuna mamilioni ya blocks katika blockchain. Na ikitokea umefanya muamala mwingine either umetuma au kupokea fedha basi block nyingine itajitengeneza (block E) ambayo itakuwa na data zako zote (umetuma kiasi gani, kwenda kwa nani, muda gani) na itachukua HASH za block D na kuongezwa kwenye chain ⛓️

             *SIFA NA FAIDA ZA TEKNOLOJIA YA BLOCKCHAIN*

1.*Peer to peer* ```transactions: Blockchain ni mfumo ambao watu wanaweza kutumiana fedha ulimwenguni kote bila kuwepo mtu kati (third part) kama Bank, Mtandao wa simu, Taasisi, n.k. Mara zote uwepo wa mtu kati hupelekea kutokuaminiana na kutapeliana!``` 

2. *Low network Fee:* ```Blockchain imeondoa makato makubwa ambayo mtu anayapata pindi anapotuma fedha kwenda sehemu nyingine``` . 

3. *Transparency:* ```Blockchain imeleta uwazi wenye usiri ndani yake ambao unampa usalama mtumiaji, mfano leo hii ukiwa na Billion moja bank serikali itatakiwa ikutambue wewe ni nani mwenye hizo pesa na chanzo chako cha mapato kichunguzwe lakini kupitia Blockchain unaweza kuhifadhi fedha nyingi sana bila mtu yeyote kujua wala kukuuliza.``` 

4. *High security:* ```Usalama na ulinzi wa Blockchain ni mkubwa zaidi kuliko mifumo mingine yote, mfano ni vyepesi sana wadukuzi kudukua centralized system lakini sio decentralized system. Vilevile ni vyepesi taasisi hiyo kuungua, kuvamiwa na kuporwa fedha, kutokea kwa ulaghai ila ni ngumu hayo yote kutokea kwenye Blockchain```

5. *Time management:* ```Blockchain imekuja kuokoa muda wa kutuma fedha, leo hii ili umtumie mtu fedha aliyoko nchi nyingine wakati mwingine huchelewa kufika lakini kupitia Blockchain miamala yote hufanyika ndani ya muda mfupi tu.``` 

6. *Immutability:* Ni ```vigumu taarifa zilizopo kwenye Blockchain kubadilishwa (kughushi) maana kila kinachotokea kinaandikwa na hakibadilishwi kamwe na ndio maana blockchain inataka ianze kutumika katika upigaji kura ili kuzuia wizi wa kura``` . 

7. *Open source:* ```Blockchain ni mfumo ambao kila mtu ana uwezo wa kutengeneza program yake na kuiweka kwenye na ikaanza kutumika, ingawa baada ya hapo yeye hawezi kuendelea kuwa mmiliki Bali watumiaji wote watakuwa wamiliki halali``` 

*MATUMIZI YA BLOCKCHAIN KWA SASA*

1. *Cryptocurrencies:* ```Hizi ni sarafu mtandao, ambapo tunaweza kuzinunua, kuziuza, kumtumia mtu kama fedha na kuzihifadhi katika blockchain.``` 

 2. *Smart Contract:* ```Hizi ni application zinazowekwa ndani ya Blockchain kwa matumizi tofauti tofauti! Tutajifunza undani wake baadaye!``` 

3. *NFT's:* ```Hizi ni kazi za sanaa. Unaweza kununua na kuuza NFT zako kama picha, nyimbo n.k na ukatengeneza pesa (nitakuja kuandaa somo pia la NFT)``` 

4. *Banking and Financial:* ```Kwa sasa kuna banks zimeanza kutumia mfumo wa blockchain na nyingine ziko mbioni. 

Business: Biashara nyingi pia zimeanza kuendeshwa kwa mfumo wa Blockchain.``` 

5. *Government:* ```Serikali nyingi zimeanza kuingia katika mfumo wa blockchain, ambapo kwa sisi hapa Tanzania BOT waliambiwa na Raisi Samia wajiweke mkao wa kula ni swala la muda tu.``` 

Matumizi ni mengi mno, hapa nimefanya summary kama unahitaji kujua zaidi au kujiunga na Blockochein technology njoo inbox whatsapp au piga 0759416497

Tags:

#post

Related Habari

This site was designed with Websites.co.in - Website Builder

WhatsApp Google Map

Safety and Abuse Reporting

Thanks for being awesome!

We appreciate you contacting us. Our support will get back in touch with you soon!

Have a great day!

Are you sure you want to report abuse against this website?

Please note that your query will be processed only if we find it relevant. Rest all requests will be ignored. If you need help with the website, please login to your dashboard and connect to support

;